|
Mchungaji Matumika amelala usingizi wa mauti tarehe 14/07/2012 na mazishi yake yamefanyika tarehe 17/07/2012 jijini Mbeya.
HISTORIA FUPI YA MCHUNGAJI HAMISI EMMANUEL MATUMIKA KUZALIWA Alizaliwa mwaka 1942 kule North Pare Alioa 31/12/1967 UTUMISHI Aliajiriwa na Kanisa mwaka 1966 kama Mhasibu, South Nyanza Field Elimu alienda Bugema College 1968. Alirudi mwaka 1969 na kuwa Mhasibu South Nyanza Field Alikuwa Katibu na Mhazini Msaidizi wa Central Nyanza Field 1971 – 1972 Mwaka 1973 alikuwa Mchungaji wa Mtaa - Songea Mwaka 1985 alienda Chuoni Arusha Seminary Mwaka 1986 alikuwa Mchungaji wa Mtaa –Njombe Mwaka 1993 Alikuwa Mkurugenzi wa Huduma Mwaka 1996 - 2003 Mchungaji wa Mtaa- Njombe Mwaka 2004 – 2005 alikuwa Mchungaji wa Mtaa Mbalizi na mnamo January 2006 alipumzika kazi ya kuongoza Mtaa (alistaafu kazi) MAGONJWA Mnamo mwaka 2003 alipata ugonjwa wa Kisukari ambacho kimekuwa kinamsumbua mara kwa mara. MAUTI Tarehe 10/7/2012 alianza kuumwa tarehe 13/7/2012 alipelekwa Hospitali ya Mkoa. Tarehe 14/7/2012 asubuhi mnamo saa 3 alilala mauti.
|



